Adriane Carr

Adriane Carr (alizaliwa mnamo 1952) ni msomi, mwanaharakati na mwanasiasa katika chama cha Green Party nchini British Columbia na Kanada Pia ni diwani katika Halmashauri ya Jiji la Vancouver. [1] Mnamo 1983 hadi 1985 alikuwa mwanachama mwanzilishi na msemaji wa kwanza wa Chama cha Green Party nchini British Columbia. Mnamo 1993 Chama kilianzisha rasmi nafasi ya "Kiongozi". Katika uchaguzi wa mkoa mnamo 2005, alipata zaidi ya 25% ya kura kijijini kwake Powell River-Sunshine Coast. Mnamo Septemba 2006 alijiuzulu wadhifa wake alipoteuliwa na Kiongozi wa Shirikisho la Chama cha Green party, Elizabeth May, kuwa mmoja wa Manaibu wake wa Chama cha Green party nchini Kanada. Mapema mwaka 2006, Carr alikuwa mwenyekiti mwenza wa kampeni iliyofaulu kupata mshirika wake wa kisiasa na rafiki wa muda mrefu Elizabeth May kuchaguliwa kuwa Kiongozi.

  1. Hui, Stephen (19 Novemba 2011). "Greens' Adriane Carr elected to Vancouver city council". Vancouver, British Columbia: The Georgia Straight. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Novemba 2011. Iliwekwa mnamo 20 Novemba 2011. {{cite web}}: More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy